COSTECH Yatoa Mil. 480 kwa WATAFITI Wanne

SERIKALI kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), imetoa sh milioni 480 kwa watafiti wanne kutoka Vyuo Vikuu hapa nchini kwa ajili ya kutekeleza miradi waliyoomba.

Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Dkt Bugwesa Katale alieleza hayo wakati wa kukabidhi mfano wa hundi kwa watafiti hao baada ya kupewa mafunzo na COSTECH.

COSTECH Yatoa Mil. 480 kwa WATAFITI Wanne

Dkt Katale alisema fedha hizo za Serikali zilikuwa na uwezo kutengwa ili zifanye kitu kingine lakini watafiti hao wameaminiwa na kupewa kila mmoja sh milioni 120 ili aweze kutekeleza mradi aliomba.

“Wakati wa utekelezaji wa miradi yetu kama tutakutana na changamoto yoyote ni vizuri mkauliza ili kufanya miradi yetu vizuri,” alisema.

Naye Mratibu wa Mtafiti Mwandamizi COSTECH, Bestina Daniel alisema kuwa watatafiti walionufaika wawili wametoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambao ni Dkt Julius Woiso na Dkt Mesi Ilomo, na wengine wawili wametoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), hao ni Dkt Makarius Lalika na Dkt Ramadhan Majubwa.

Alitaja maandiko ya miradi iliyoshinda na kupewa fedha hizo kuwa ni samaki wadogo wadogo kwa uhakika wa chakula na lishe bora Afrika na utengenezaji wa viuatilifu vya kibaiolojia kwa muunganiko wa vidudu rafiki kwa ajili ya udhibiti wa ugonjwa wa mnyauko katika nyanya kwa chakula salama.

Mradi mwingine unaangalia uchafuzi unaathiri vipi viumbe vya majini na binadamu pamoja na jinsi ya kupunguza athari kwa kutumia mchanganyiko wa wadudu rafiki.

Watafiti kutoka nchi za Kusini na Kaskazini walituma maandiko 207, kati ya hayo watanzania walituma maandiko 123. Hivyo miradi 16 ilishinda kati ya hiyo minne ni ya watanzania. #wizarayaelimu

Share this page